POSITIVE EYE CO. LTD
 
TUKIWA TUNATOA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA PAMOJA NA KUHAMASISHA KUHUSU FURSA ZA KIJASIRIAMALI KIJIJI CHA RIRODA WILAYA YA BABATI. (UNAWEZA KUTUALIKA KWENU PIA AU KWENYE KIKUNDI CHENU TUJIFUNZE UJASIRIAMALI UKIAMBATANA NA SINEMA ZAKUELIMISHA)
 
GARI MAALUMU YA MATANGAZO NA VIFAA VYAKUONESHEA SINEMA (TUNAWEZA KUKODISHWA PIA KWA MATANGAZO MBALIMBALI YA MITAANI YAANI PROMOTION KWA GHARAMA NAFUU
 
WANAKIJIJI WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAFUNZO KWA NJIA YA SINEMA (NJIA HII IMEKUWA NA MANUFAA SANA SABABU KUONA NI KUAMINI NA KWA PICHA KUMBUKUMBU HUIFADHIKA AKILINI KWA URAHISI ZAIDI

UELIMISHAJI NA UHAMASISHAJI KWA KUPITIA VIDEO/SINEMA NA WANENAJI /WAKUFUNZI WALIYOBOBEA

Kwa kutumia wanenaji wetu waliobobea kwa maarifa, uzoefu na wenye karama yakufundisha na kuhamasisha huwa tunatoa huduma za mafunzo mbalimbali kwa watu binafsi, jamii,vijiji, vikundi kama VICOBA,SACCOSS,Mashuleni, Vyuoni, makanisani, taasisi mbalimbali na Makampuni (kuongeza morali za wafanyakazi kufanya kwa ubora), na katika semina/makongamano mbalimbali tunazoandaa na zakualikwa. Katika kuboresha nakuhakikikisha washiriki, wanafunzi, wajasiriamali na wateja wetu tunaowapatia elimu na kuwahamasisha wanaelewa kwa ubora unaotakikiwa nakuhamasika kiuhalisia mafunzo yetu kwa sehemu kubwa huyaambatanisha na video/sinema za miradi mbalimbali ya maendeleo ya wajasiriamali waliofanikiwa kibiashara,kilimo cha kisasa na kiviwanda, pia tunatoa elimu kwa njia hii kwa Nyanja nyingine zote tunazopatiwa/kukodiwa kufanya ikiwemu elimu za afya,kuzuia magonjwa mbalimbali,utunzaji mazingira na rasilimali zingine, N.K na njia hii sisi huitumia kutokana na ukweli tuliouthibitisha kama mtu mmoja alivyowahikusema kuwa“ Picha huzungumza maneno elfu moja” yaani akimaanisha kwa kutumia picha mtu huelewa kiurahisi na haraka zaidi na kumbukumbu kubaki kichwani kirahisi na pia mtu mwingine akasema “Kuona ni kuamini” hivyo njia hii huwa na mguso mzuri sana kuleta mabadiliko kwa jamii na kwa walengwa sababu kwa kuona mazingira ambayo mjasiriamali mwenzie amewezakufankiwa na akayalinganisha na mazingira yake binafsi basi ni rahisi kuamini nakuhamasika kuwa hata na yeye anaweza.

 

JUKWAA LA MAFANIKIO.

SEMINA/KONGAMANO LA KILA MWEZI

Pamoja na utayari wetu kwa yeyote (Vikundi au Mtu binafsi) kutualika kufanya uelimishaji na uhamasishaji katika Nyanja tofauti kama tulivyodokeza hapo juu.

Sisi pia chini ya mradi tulioupa jina la SUCCESSWOOD PROJECT huandaa semina kila mwezi ijulikanayo kama JUKWAA LA MAFANIKIO ambapo ni tukio lenye kuzingatia maadili na lakuaminika linalofanyika kila mwezi mara moja kwa lengo la kukutanisha watu mbalimbali wapenda maendeleo waliodhamiria kupiga hatua ya mafanikio maishani pamoja na familia zao, ili kuboresha kesho yao na ya kizazi chao. Jukwaa hili litatoa fursa ya kuhamasishwa, kuelimishwa, kufunguliwa macho kuona fursa, kuburudishwa nakufahamiana na watu wenye malengo yanayofanana na kwa maslahi ya mitandao yakibiashara na kujamii. Jukwaa hili kwa ujumla limelenga kuwawezesha washiriki kukua na kuimarika kiroho, kiakili/mitazamo , kiuchumi na kiafya,

 

HAYA HAPA CHINI NI MAENEO/MADA AMBAZO HUFUNDISHWA KATIKA JUKWAA HILI LA MAFANIKIO

 

NAMNA YAKUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO

Je unajua kusudi la maisha yako? Kwanini huko hapa duniani? Njoo tujifunze namna utagundua kusudi lakuumbwa kwako, sababu hilo ndiyo ajira yako itakayokupa mafanikio yenye amani na utoshalevu ya kifedha na kila nyanja

 

KUWA NA JICHO CHANYA LAKUONA FURSA KILA UWAPO.

Katika kipindi hiki ambacho wengi wanalalamika ugumu wa kupata pesa, njoo tujifunze namna yakuwa na jicho chanya lakuona fursa nyingi zilizo katika jamii na ktk kila changamoto au tatizo unalopitia.

 

KUJIFUNZA KUTOKA KWA WALIOFANIKIWA

Tutakuwa na mahojiano ya live moja kwa moja na mjasiriamali mkubwa aliyefanikiwa ambapo pia tutajifunza siri zakuwa mjasiriamali mwenye mafaikio ya kweli na yatakayodumu.

Pia kwa wanataaluma huwa tunakuwa na mahojiano na watu waliofanikiwa katika Nyanja mbalimbali ili kuwatia moyo ambao bado wako mashuleni, vyuoni na hata makazini kukua kitaaluma na utendaji.

 

KUIBUA HAZINA YA UBUNIFU ULIOKO NDANI YAKO.

Pia tutakuwa na somo maalum la namna yakuchokoza na kuamsha uwezo uliopo ndani yako wakibunifu, kutengeneza na kuzaa vitu na mambo mbalimbali makubwa yatakayobadili biashara yako, jamii yako na dunia kwa ujumla huku ukitengeneza pesa.

 

KUSHIRIKISHANA FURSA ZA MIRADI YA MAENDELEO.

Tutajifunza tekinologia mpya ya ufugaji wa samaki kisasa kwa kutumia eneo dogo la mita 2 kwa 4 tu utaweza kufuga hadi samaki 1000,Na pia kilimo cha kisasa chakutumia maji kidogo kwa matokeo makubwa.

 

BURUDANI YA FILAMU ITAKAYOKUFIKIRISHA NA ITAKAYOTUJENGA KIROHO KWA MAFANIKIO YAKO  YA SASA NA BAADA YA KUFA.

Mwisho tutatazama pamoja filamu maalum itakayotujenga mafanikio yetu yawe ya hapa duniani na ya milele.

Ukweli ni kuwa katika maisha ya mwanadamu jambo lakushangaza huwa tunajiandaa kwa mambo mengi tusiyokuwa na uhakika nayo, Mfano: Tunajiandaa kwa safari lakini uhakika wakufika salama hatuna, Tunaandaa malazi lakini uhakika wakuamka asubuhi hatuna, Tunajiandaa kwenda shule lakini uhakika wakuhitimu hatuna, N.K, JAMBO MOJA AMBALO KILA MTU ANAUHAKIKA NALO NI KUWA SIKU MOJA ATAKUFA na hilo sio lakubaatisha, Chakushangaza badala ya watu kuchukua muda kujiandaa kwa jambo hili la uhakika litakalotokea maishani mwao na kuwa maamuzi ya watakayoishi hapa duniani yataamua mustakabali wa maisha yao baada ya kifo,Badala yake watu wamekuwa wakichukulia maamuzi haya kwa wepesi na hata kurithi mistakabali ambayo hawajaichunguza vyakutosha ili kujiridhisha kama itawapeleka mahali salama baada ya kifo. Hakika watu watakuwa na mashaka na akili za mtu yeyote anayeona moto unaunguza nyumba yake na hakika unaelekea kumteketeza na yeye halafu asifanye lolote kupata namna/njia salama yakuokoa maisha yake.

NB. Katika matukio haya huwa tunakuwa tukiuza vitabu, majarida, cd , dvd mbalimbali zakuwezakuwaongezea washiriki maarifa ili kuboresha maisha yao.

 

SAFARI/MATEMBEZI YA KIJASIRIAMALI KWENDA KUJIFUNZA NCHI JIRANI.

Kama mwendelezo wa jukwaa hili la mafanikio mara 3-4 kwa mwaka huwa tunaandaa safari ya matembezi yakijasiriamali kwa watu wanaohudhuria majukwaa haya/semina hizi na kwenda katika nchi mojawapo, baadhi au zote za umoja wa afrika mashariki ili kujionea fursa mbalimbali na namna tofauti yakufanya mambo katika nchi nyingine ili kupanua ubunifu wetu,Kupanua wigo wauelewa wetu wa namna mambo yanavyofanyika kwa namna tofauti katika nchi nyingine, kuwa na jicho tofauti lakutazama fursa na mazingira yanayotuzunguka.

 

KILA MWEZI HUWA NA MAMBO MAPYA NA FURSA MPYA ZAKUJIFUNZA  USITHUBUTU KUKOSA

 

UNAWEZAKUWAHI NAKUSHIKA NAFASI YAKO USIKOSE TUKIO HILI KWA MWEZI HUU AU UJAO KWA KUPIGA 0745 122229

 

WAHUDHURIAJI WA MARA YA KWANZA HULIPA Tshs 15,000/= TU, NA BAADA YA HAPO UTAKUWA TAYARI MWANAJUKWAA LA MAFANIKIO NA UTAKUWA UKILIPA Tsh 10,000/= TU SEMINA INAPOANDALIWA NA UKASHIRIKI.

 

GHARAMA ZA MATEMBEZI/SAFARI  ZA KIJASIRIAMALI KWA NCHI JIRANI ZITAKUWA ZINATANGAZWA KUTOKANA NA UREFU WA SAFARI HUSIKA KWA KIPINDI HUSIKA.

 

KWA KUTUMIA NAMBA HIYOHIYO HAPO JUU  UNAWEZA KUTUITA KUJA KUTOA ELIMU NA KUHAMASISHA KIKUNDI CHENU KUHUSU UJASIRIAMALI, MIRADI YA MAENDELEO NA MADA NYINGINE KAMA ZILIVYOAINISHWA HAPO JUU.